Sunday, April 17, 2016

FULL TIME: BARCELONA 1 v 2 VALENCIA, BARCA YACHINJWA TENA LEO! MESSI APIGA BAO LAKE LA 500


Mbele ya Mashabiki 88667 Barca wamepoteza tena mchezo kwa kufungwa bao 2-1 na Timu ya Valencia kwenye Uwanja wa Nyumbani Estadio Camp Nou, Spain. Barcelona bao lake limefungwa kipindi cha pili dakika ya 63 na 
Lionel Messi huku likiwa bao lake la 500 kisoka.


Kipigo chao cha 4 katika Mechi 5 zilizopita na kuacha mbio za Ubingwa wa La Liga kuwa wazi kabisa.
Wakiwa kwao Nou Camp, Barca walikuwa wako 2-0 nyuma wakati wa Haftaimu kutoka kwa Valencia Timu ambayo Wiki kadhaa nyuma waliitwanga 7-0.
Bao za Valencia hapo Jana zilifungwa na Ivan Rakitic aliejifunga mwenyewe akitaka kuokoa Krosi ya Guilherme Siqueira katika Dakika ya 26 na Santi Mina kuipa Valencia Bao la Pili Dakika ya 46.
Lionel Messi aliipa Barca Bao lao pekee katika Dakika ya 63 akifuta ukame wa kutofunga katika Mechi 5 na hilo kuwa Goli lake la 500 katika maisha yake ya Soka.
Hadi Mechi inaisha Barca 1 Valencia 2.
Mwanzoni mwa April, Barca walikuwa Pointi 9 mbele kileleni mwa La Liga lakini vipigo mfululizo kwa Barcelona kwenye La Liga vilianza na kile cha El Clasico toka kwa Real Madrid na kufuata vile toka kwa Real Sociedad na hiki cha Valencia huku kati kilijichimbia kile cha kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI walipopigwa na Atletico Madrid.
Lakini Barca bado wanaongoza La Liga wakiwa Pointi sawa na Atletico Madrid huku Real wakiwa Pointi 1 nyuma yao na hali hii inazidisha uhondo wa La Liga ambayo inaelekea ukingoni zikibakia Mechi 5 kwisha.
Jumatano Timu zote hizi 3 zote dimbani kwa Barca kucheza na Deportivo La Coruna, Atletico kuwa Ugenini na Athletic Bilbao wakati Real wako kwao kucheza na Villareal.