Saturday, April 16, 2016

FULL TIME: CHELSEA 0 v 3 MANCHESTER CITY, BLUES WAFA KWAO STAMFORD BRIDGE! AGUERO AWAPIGA HAT-TRICK! CONTE UNA KAZI KUBWA...!

MSIMU wa mbaya kwa waliokuwa Mabingwa wa BPL, Ligi Kuu England, Chelsea, umeendelea Leo walipotandikwa kwao Stamford Bridge Bao 3-0 na Manchester City.

Bao zote za Mechi hii zilifungwa na Straika Hatari wa Argentina, Srgio Aguero, alietingisha nyavu Dakika za 33, 54 na Penati ya Dakika ya 80 ambayo ilitokana na kuangushwa na Kipa Thibaut Courtois ambae alipewa Kadi Nyekundu kwa kosa hilo.

Matokeo haya yamewaweka City Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Vinara Leicester City ambao Jumapili wako kwao King Power Stadium kucheza na West Ham.
Chelsea wamebaki Nafasi ya 10.