Saturday, April 16, 2016

FULL TIME: GETAFE 1 vs 5 REAL MADRID


REAL MADRID wameitwanga Getafe Ugenini Uwanjani Coliseum Bao 5-1 na kupanda hadi Nafasi ya Pili ya La Liga wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Barcelona ingawa wamecheza Mechi 1 zaidi.

Bao za Leo za Real zilifungwa na Wachezaji Watano tofauti na kubwa ni Cristiano Ronaldo kufunga Bao ambalo linazidi kumpaisha katika Ufungaji Bora wa La Liga na sasa yupo Bao 5 mbele ya Luis Suarez wa Barca.


Ushindi huu wa Real hii leo ni presha kubwa kwa Barca ambao hawajashinda katika Mechi 3 za La Liga zilizopita ambazo walitoka Sare Ugenini 2-2 na Villarreal, kufungwa 2-1 na Real ndani ya Camp Nou na kisha kufungwa 1-0 Ugenini na Real Sociedad.

Pia, Juzi walichapwa 2-0 na Atletico Madrid na kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI, Kombe ambalo wao walikuwa Mabingwa Watetezi.