Sunday, April 24, 2016

FULL TIME: LEICESTER CITY 4 v 0 SWANSEA CITY, ULLOA NA WENZAKE WAINUSISHA FOX UBINGWA!

Ndani ya Uwanja wa King Power Stadium, Leicester, Leicestershire
wakicheza mchezo wa Ligi Kuu England Vinara wa Ligi hiyo pendwa Leicester City wakichezeshwa na Mwamuzi  M. Clattenburg wamefanya kweli kwa kuifunga bao 4-0 Timu ya Swansea City na kuzidi kupaa kileleni mwa Ligi mbele ya Mashabiki 31,962
Mabao ya Leicester City yamefungwa na  R. Mahrez dakika ya 10',
L. Ulloa 30', na dakika ya  60 na bao la mwisho la nne limefungwa na M. Albrighton dakika ya 85'


LEICESTER CITY wamekaribia kabisa kutimiza miujiza ya Msimu huu ya kutwaa Ubingwa wa BPL, Ligi Kuu England, baada ya kuidunda Swansea City 4-0 kwenye Mechi waliyocheza kwao King Power Stadium.

Leicester sasa wapo Pointi 8 mbele ya Timu ya Pili Tottenham ambayo ndio pekee inaweza kuwapiku kutwaa Ubingwa baada ya Pointi za Leo za Leicester kuwahakikishia kuwa Timu za 3 na za 4, Man City na Arsenal, hawawezi kuwakuta.
 

Wakicheza bila ya Staa na Mfungaji wao mkubwa, Straika Jamie Vardy, alie Kifungoni kwa Mechi 1, Leicester walipeleka Bao zao kupitia Riyad Mahrez, Dakika ya 11, Leonardo Ulloa, Dakika ya 30 na 60, na Marc Albrighton, Dakika ya 85.

Leicester wanahitaji Pointi 5 katika Mechi 3 zilizobaki kutwaa Ubingwa na hii ikiwa Tottenham watashinda Mechi zao zote.


Kesho, Jumatatu Usiku, Tottenham wako kwao White Hart Lane Jijini London kucheza na West Bromwich Albion na wakiteleza tu basi Leicester City wanaweza kuwa Mabingwa Jumapili Mei 1 wakiibwaga Man United huko Old Trafford.