Saturday, April 16, 2016

FULL TIME: MANCHESTER UNITED 1 v 0 ASTON VILLA, MARCUS RASHFORD AIZAMISHA VILLA OLD TRAFFORD!

Aston Villa wameshushwa Daraja kutoka Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza toka 1987 baada ya kufungwa 1-0 na Manchester United Uwanjani Old Trafford hii Leo. Bao pekee lilifungwa na Chipukizi Marcus Rashford baada kupokea Pasi kutoka kwa Antonio Valencia ambae nae alikontroli vizuri pande refu toka kwa Kepteni Wayne Rooney alieanza Mechi yake ya kwanza tu baada ya kuwa nje kwa Miezi Miwili akijiuguza Goti.

Bao hilo ni la 7 kwa Rashford katika Mechi 12 alizoichezea Man United Msimu huu.
Kwa Aston Villa hiki ni kipigo chao cha 9 mfululizo kilichohakikisha wanashuka Daraja kwa mara ya 5 katika Historia yao.