Sunday, April 24, 2016

FULL TIME: SUNDERLAND 0 v 0 ARSENAL, GUNNERS YAWA BUTU TENA LEO!


Sunderland Leo wakiwa kwao Stadium of Light wametoka Sare 0-0 katika Mechi ya BPL, Ligi Kuu England, na kujinasua toka Timu 3 za mkiani huku Arsenal wakibaki Nafasi ya 4.

Kila Timu hii Leo ilipata nafasi za kufunga lakini zikapotea na kila Timu ililalamika kunyimwa Penati ambazo Siku nyingine na mahala pengine zingetolewa.
Arsenal wapo Nafasi ya 4 wakiwa wamecheza Mechi 35 na wa wana Pointi 64 sawa na Man City ambao wako juu yao huku nafasi ya 3 ikishikwa na Tottenham waliocheza Mechi 34 na wana Pointi 68 wakati Leicester ni Vanara wakiwa na Pointi 73 kwa Mechi 34.

Sunderland sasa wapo Nafasi ya 17 wakiwa na Pointi 31 kwa Mechi 34 sawa na Norwich City ambao wamezidiwa ubora wa Magoli na wapo Nafasi ya 18 ambayo pamoja na Nafasi za 19 na 20, zinazoshikwa na Newcastle na Aston Villa ambayo imeshashuka Daraja, ndizo Nafasi 3 za kushushwa.