Sunday, April 10, 2016

FULL TIME: TOTTENHAM HOTSPUR 3 - 0 MANCHESTER UNITED


BAO 3 za Kipindi cha Pili ndani ya Dakika 6 zimeweka hai matumaini ya Tottenham ya kuwakamata Vinara wa BPL, Ligi Kuu England, Leicester City, walipoichapa Man United Bao 3-0 huko White Hart Lane Jijini London hii Leo.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa Tottenham dhidi ya Man United tangu 2001 Uwanjani hapo na umewaweka wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 7 nyuma ya Lecester.

Bao za Spurs zilifungwa Dakika za 70, 74 na 76 kupitia Dele Alli, Toby Alderweireld na Erik Lamela.
Kipigo hiki kimewaacha Man United Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 4 Man City na kuyafanya matumaini yao kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao kufifia na pia kulianzisha upya sakata la Mashabiki kumtaka Meneja Louis van Gaal ang’oke.
Sir Bobby akijionea..Juan MataCarrickMchezaji wazamani wa Spurs  Gary LinekerDelle Alli