Wednesday, April 20, 2016

HABARI NJEMA KWA VIJANA: AZAM TV IMEWASOGEZEA FURSA MIKONONI MWENU


Habari njema kwenye tasnia ya filamu Bongo ni uzinduzi wa mradi wa kusaka vipaji vya waigizaji pamoja na ma-camera person, mradi huo unakwenda kwa jina la ‘Kiwanda cha Filamu’.
Deal hilo linasimamiwa na Azam TV kupitia channel yake ya ‘Sinema Zetu’, kitu kizuri kuhusu mpango huo ambao umelenga kuwatoa wasanii chipukizi ni uwepo wa mwigizaji mkongwe na maarufu kwenye Bongo Movies Susan Lewis ‘Natasha’ pamoja na Issa Mbura ambaye amejizolea umaarufu baada ya kung’ara kwenye movie inayoiitwa ‘Home Coming’.

Mr. Mbura na Natasha watakuwa ni majaji watakaosimamia zoezi zima la kuwapata waigizaji wenye vipaji pamoja na camera persons watakaofuzu katika shindano hilo