Thursday, April 7, 2016

JUMA NATURE AJIPIGA PINGU JEMBEKA FESTIVAL 2016 JIJINI MWANZA

Wakati joto la burudani likiendelea kupanda Kanda ya Ziwa kwa vipindi, habari na matangazo yenye mguso na jamii kupitia kituo cha redio Jembe Fm kinachorusha matangazo yake kutoka jijini Mwanza katika masafa ya FM 93.7, nayo safari ya kuelekea Tamasha kubwa la burudani linalojulikana kama JEMBEKA FESTIVAL 2016 linaufanya ukanda huo joto lake kupanda zaidi kiasi cha kusababisha presha kwa wadau wa Kanda husika. 

Jumamosi, May 21,2016 ndiyo siku litakapopigwa Tamasha la Jembeka Festival ikiwa ni Msimu wa Pili. Utamu wa Jembeka Festival unaanzia kwa Mkali Neyo kutoka nchini Marekani.