Tuesday, April 12, 2016

KEPTENI JOHN TERRY AGHARAMIA MAZISHI YA SHABIKI WA CHELSEA MTOTO WA MIAKA 8 ALIEFARIKI KWA KANSA!

KEPTENI wa Chelsea John Terry amelipia gharama zote za Mazishi ya Shabiki wa Chelsea Mtoto mdogo wa Miaka 8 aliefariki kwa ugonjwa wa Saratani ya Damu.
Terry alijitolea Pauni 1,600 kwa Familia ya Mtoto Tommi Miller ambae aliwahi kukutana nae Mwaka Jana.
Terry alisema ameumia sana roho aliposikia Tommi amefariki.
Mama Mzazi wa Tommi, Ruth Miller, ambae anaishi Thorpe Way, Cambridge huko England, amesema wamefarijika mno na msaada wa Terry na wanapanga pia kuweka Jiwe maalum kwenye kaburi la Tommi kwa kutumia baadhi ya Fedha hizo za msaada wa Terry.
Mama huyo wa Tommi amesema wanasikia fahari kuwa Terry amemkumbuka Tommi.

Tommi aligundulika ana Kansa ya Damu akiwa na Miaka Mitatu tu lakini juhudi zote za kumponya zilishindikana.
Mazishi ya Tommi yanatarajiwa kuwa Alhamisi na wale wote watakaohudhuria watavaa Jezi za Chelsea au Cambridge United.