Sunday, April 3, 2016

LEO MAN UNITED vs EVERTON

LIGI KUU ENGLAND, BPL, inaendelea Leo kwa Mechi 2 tu ambapo Vinara wake Leicester City wapo kwao King Power Stadium kucheza na Southampton na huko Old Trafford Manchester United watacheza na Everton.
Leicester wanaongoza BPL wakiwa na Pointi 66 kwa Mechi 31 wakifuatiwa na Tottenham Hotspur wenye Pointi 62 kwa Mechi 32.
Southampton, ambao ni maarufu kama ‘Watakatifu’ wapo Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 47.
Huko Old Trafford, Man United, ambao wapo Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 50 kwa Mechi 30, wanacheza na Everton ambao wapo Nafasi ya 12 wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 29.
Mapema Msimu huu, Mwezi Oktoba, Man United waliichapa Everton 3-0 huko Goodison Park kwa Bao za Schneiderlin, Herrera na Rooney.

Kwenye Mechi ya Leo, Man United itamkosa Kiungo wa Germany Bastian Schweinsteiger ambae Wiki iliyopita aliumia Goti akiwa na Timu ya Taifa ya Germany. Nao Ander Herrera na Ashley Young wamepona na wanaweza kurejea Kikosini lakini Phil Jones yupo nje wakati Kepteni Wayne Rooney na Luke Shaw watarejea Mazoezini Wiki ijayo baada ya kupona matatizo yao.
Everton wanategemewa kuwa nae tena Beki John Stones pamoja na Bryan Oviedo aliepona ugonjwa wake na pia Kevin Mirallas aliemaliza Kifungo lakini watamkosa Kiungo wao hodari Gareth Barry ambae anaanza kutumikia Kifungo cha Mechi 2. Majeruhi wa Everton ambao watakosekana Leo ni Steven Pienaar, Tony Hibbert na Tyias Browning.