Saturday, April 9, 2016

FULL TIME: WEST HAM UNITED 3 v 3 ARSENAL, CARROLL APIGA HAT-TRICK LEO GUNNERS WAKICHOMOA NA KUUMALIZA KWA SARE!

Dakika ya 52 Carroll alipiga Bao la 3 na kukamilisha Hetitriki yake ya ndani ya Dakika 9 tu.
Hat-trick ya ndani ya Dakika 9 ya Straika wa West Ham Andy Carroll Leo huko Upton Park imekuwa pigo kubwa kwa Arsernal katika mbio zao za Ubingwa walipotangulia 2-0 na kuambua Sare ya 3-3 na West Ham.
Arsenal walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 18 baada ya pasi ya Iwobi kumkuta Mesut Ozil aliemalizia vizuri na la pili kufungwa Dakika ya 35 kupitia Alexis Sanchez kwa pasi iliyotoka kwa Iwobi.
West Ham walifufuka na kufunga Bao lao la kwanza Dakika ya 44 kwa Kichwa cha Andy Carroll alieunganisha krosi ya Cresswell na kupata Bao la Pili Dakika ya 47 kupitia tena Andy Carroll ambae aliunganisha Mpira wa Kona iliyoooshwa na kumkuta Mark Noble alieurudisha tena Golini na kumkuta Carroll aliepiga Shuti la kwanza ambalo lilizuiwa na kuachia kigongo cha pili na kumparaza Beki na kumhadaa Kipa Ospina.
Andy Carroll celebrates scoring the third goal for West Ham to complete his hat trickHadi Mapumziko, West Ham 2 Arsenal 2.
Dakika ya 52 Carroll alipiga Bao la 3 na kukamilisha Hetitriki yake ya ndani ya Dakika 9 tu.
Arsenal walisawazisha na kuambua Sare ya 3-3 katika Dakika ya 70 kwa Bao la Laurent Koscielny.
Matokeo haya yamezibakisha Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Leicester City na West Ham kuwa Nafasi ya 6.

Ozil dakika ya 18 anaifungia bao Arsenal