Friday, April 15, 2016

MALINZI AMPONGEZA RAVIA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Ravia Idarous Faina wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi ulifanyika jana katika ukumbi wa Gombani, Pemba.
Katika salamu zake, Malinzi amesema anampongeza Ravia kwa kuchaguliwa kwake, na hiyo imeonyesha imani kubwa kwa waliomchagua kuongoza ZFA katika kipindi kingine.
Malinzi amewapongeza vingozi wote wapya waliochaguliwa katika uchaguzi huo, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika shughuli zote za maendeleo ya mpira wa miguu.

Uchaguzi wa kupata viongozi wa ZFA ulifanyika jana Gombani kisiwani Pemba, ambapo Ravia aliibuka mshindi na kutetea nafasi yake, nafasi ya makamu wa rais Ugunja kienda kwa Mzee Zam Ali, na makamu wa Pemba ikichukuliwa na Ali Mohamed Ali.