Thursday, April 28, 2016

MANCHESTER UNITED WAFUKUZIA DILI YA KINDAWA BENFICA SANCHEZ

MANCHESTER UNITED wanatarajia kumchukua Tineja wa Benfica ya Portugal Renato Sanchez kwa Dau la Pauni Milioni 46 ambalo litalipwa kwa awamu.
Sanchez, mwenye Miaka 18, alianza kuichezea Timu ya Kwanza ya Benfica Mwezi Oktoba Mwaka Jana na kung'ara sana kiasi cha Benfica kuamua kumpa Mkataba mpya bora ambao utamalizika 2021 huku ukiwa na Kipengele mahsusi kuwa Klabu lazima ilipwe Pauni Milioni 46 ikiwa Klabu nyingine itataka kumnunua kabla Mkataba huo haujaisha
Inaaminika Man United na Benfica zimeafikiana na Dau hilo ambalo litalipwa kidogo kidogo kwa awamu kwa Kipindi cha Miaka Minne kama ilivyomnunua Chipukizi Anthony Martial Mwaka Jana.
Licha ya Klabu Vigogo kama vile Arsenal, Real Madrid, Paris Saint-Germain, Bayern Munich na Man City kumwania Kijana huyo, Man United wanaonekana wako mbele kumnasa kutokana na uhusiano wao mzuri na Wakala maarufu Jorge Mendes ambae anamwendesha Renato.

Renato, aliezaliwa Lisbon, Portugal kwa Wazazi wa Visiwa vya Afrika Cape Verde, ameichezea Benfica Mechi 28 na kufunga Bao 2 na kumfanya aitwe kwenye Timu ya Taifa ya Portugal ambayo amechezea Mechi 2.
Uchezaji murua na umri mdogo wa Renato unemfanya awe mbadala mzuri wa Viungo 'Wazee' wa Man United, Michael Carrick, ambae atatimiza Miaka 35 Mwezi Julai na Bastia Schweinsteiger mwenye Miaka 32.
Wachambuzi wanahisi Renato ndie mrithi safi wa Kiungo Lejendari Paul Scholes aliestaafu Miaka Mitatu iliyopita na kuacha pengo ambalo halijazibwa ipasavyo.