Saturday, April 23, 2016

MANCHESTER UNITED WAKIFANYA MAZOEZI KUJIANDAA NA FA CUP DHIDI YA EVERTON WEMBLEY JUMAMOSI


Manchester United Leo walinaswa wakifanya Mazoezi yao ya mwisho kwenye Kambi yao ya Mazoezi ya AON Complex huko Carrington Jijini Manchester kabla kusafiri kwenda London kwa ajili ya Nusu Fainali ya FA CUP na Everton.
Jana, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, alitoboa kuwa Timu haina Majeruhi yeyote baada ya Mechi ya Jumatano Uwanjani Old Trafford walipoifunga Crystal Palace 2-0.
Wasiwasi ulikuwa kwa Straika Chipukizi, Marcus Rashford, amabe alitolewa Kipindi cha Pili kwenye Mechi na Palace baada ya kuumizwa na ngwala ya Beki wa Palace Adrian Mariappa lakini Kijana huyo wa Miaka 18 Leo alionekana akipiga tizi kwa furaha pamoja na Chipukizi mwenzake Timothy Fosu-Mensah na kina Marouane Fellaini na Jesse Lingard wanaweza kupona na kurejea Kikosini.