Thursday, April 28, 2016

MASHABIKI WA ARSENAL BADO WAMKAZIA UZI AONDOKE ARSENE WENGER! WAMTAKA DIEGO SIMEONE

Diego Simeone aliiongoza Klabu yake ya Spain Atletico Madrid jana usiku  na kuwafunga Vigogo wa Germany Bayern Munich 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Mashabiki wengi wa Arsenal wakavamia Mtandao wa Twitter kumshambulia Meneja wao Arsene Wenger.
Mashabiki hao wakaposti na kumtaka Wenger aondoke na badala yake Raia wa Argentina, Diego Simeone, ashike hatamu kama Meneja wa Arsenal ambayo chini ya Wenger haijatwaa Ubingwa wa England tangu 2004 na wala haijabeba UEFA CHAMPIONS LIGI hata mara moja.

Himaya ya Wenger, ambayo Msimu huu imetikisika sana toka kwa presha ya Wadau wao kutokana na kusambaratika kwa mbio zao za Ubingwa walizoanza vyema, imeduma huko Arsenal tangu Mwaka 1996.