Sunday, April 10, 2016

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA ATOA MAFUNZO KWA WATOTO WA KITUO CHA MICHEZO CHA JAKAYA KIKWETE YOUTH PARK

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (kulia), akiwaelekeza jinsi ya kucheza mpira wachezaji wa Timu ya vijana waliochini ya miaka 20 ya Sunderland alipotembelea Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo Kidongo Chekundu Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana. Kanu yupo nchini kwa ziara ya siku tano kwa mwaliko wa Kampuni ya StarTimes Tanzania ambapo jana alitoa msaada wa vyakula, magodoro, sabuni na vyombo vya matumizi ya jikoni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi ya Majimatitu ya Mbagala wilayani Temeke