Monday, April 4, 2016

MPYAA!!! ANTONIO CONTE MENEJA MPYA CHELSEA

Chelsea imeteua Bosi wa Timu ya Taifa ya Italy Antonio Conte kuwa Meneja wao mpya.
Conte, mwenye Miaka 46 na aliewahi kuwa Kocha Mkuu wa Juventus, ataanza kazi na Chelsea kwa Mkataba wa Miaka Mitatu baada ya Fainali za EURO 2016 kumalizika.
Kwenye EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya ambalo litachezwa huko France na kwisha Julai 10, Conte ataiongoza Timu ya Taifa.

Akiongelee uteuzi wake huo, Conte amesema: "Nifahari kuwa Kocha wa Nchi yangu na ni wadhifa wa kuvutia kama huu wa Chelsea ndio unaweza kufuatia huo!"
Guus Hiddink, ambae ndie Kaimu Meneja tangu Desemba alipofukuzwa Jose Mourinho, ataendelea na wadhifa huo hadi mwishoni mwa Msimu.
Conte, ambae alitwaa Ubingwa wa Italy wa Serie A katika kila Mwaka alipokuwa Bosi wa Juventus kwa Miaka Mitatu, anakuwa Mtaliana wa 5 kuwa Meneja wa Chelsea, kufuatia Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na Roberto di Matteo.

Kibarua kikubwa kwa Conte ni kuijenga upya kupigania Ubingwa wa England baada ya kuutwaa Msimu uliopita chini ya Mourinho na Msimu huu Timu kufanya ovyo kiasi ambacho imeshindwa kutetea Taji lao na hata kuwemo 4 Bora ni kitu kisisichowezekana.