Saturday, April 9, 2016

MWANAMUZIKI NDANDA KOSOVO AFARIKI DUNIA

bukobasports.comMwanamuziki wa dansi nchini Ndanda Kosovo afariki dunia Hosptali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa Matibabu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanamuziki mwenzake Kardinal Gento,Ndanda alikuwa alisumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo maradhi yaliyopelekea kulazwa katika hospitali ya Mwananyamala na baadaye alihamishiwa katika Hosptali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya Matibabu. Hadi mauti yanamkuta Ndada alikuwa akifanya shughuli za muziki kama msanii wa kujitegemea ‘Solo Artist’ pamoja na shughuli za kibiashara.