Tuesday, April 19, 2016

PSG WAELEKEZA NGUVU KUMPATA JOSE MOURINHO!

Paris Saint-Germain wanamnyemelea Jose Mourinho kutaka awe Meneja wao kwa ajili ya Msimu mpya ujao.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari huko Ulaya, inaaminika Mwenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, ameanzisha uhusiano wa kumvuta Mourinho huko Ufaransa kupitia Wakala wake Jorge Mendes.
Inadaiwa Mwenyekiti huyo hafurahishwi na maendeleo ya PSG katika kutwaa Ubingwa wa Ulaya na hasa baada ya kubwagwa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI Wiki iliyopita mikononi mwa Manchester City kiasi cha sasa kutaka kumbadili Meneja wa sasa Laurent Blanc.
Hata hivyo, vyanzo vinadai chaguo la Mourinho mwenyewe ni kungoja hadi mwishoni mwa Msimu huku Man United ikibaki Nambari Wani kwake.

Hadi sasa kuna kila habari kuhusu Mourinho kujiunga na Man United huku kila sehemu zinazua habari zake na wengine wakidai tayari ana Mkataba na atatangazwa mara tu baada ya Msimu huu kwisha kumbadili Mdachi Louis van Gaal.
Lakini Klabu ya Man United, kama ilivyo desturi yao, hawajasema lolote kuhusu kubaki au kuondoka kwa Van Gaal na nani mrithi wake akiondoka.
Mkataba wa Van Gaal na Man United utamalizika mwishoni mwa Msimu ujao wa 2016/17.