Monday, April 25, 2016

RATIBA UEFA CHAMPIONS LIGI-NUSU FAINALI: JUMANNE KESHO NI ETIHAD, MAN CITY vs REAL MADRID

Manchester City wataikaribisha Real Madrid katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI huku wakiwa na pigo kubwa la kumkosa nguzo yao Kiungo wao kutoka Ivory Coast, Yaya Toure.
Toure aliumia Musuli za Mguuni Jumamosi kwenye Mechi ya Ligi Kuu England wakati Citu inaibonda Stoke City 4-0 na kukosekana kwake kumethibitishwa na Meneja wa City, Manuel Pellegrini.

Kukosekana kwa Toure kunatoa mwanya kwa Viungo Wawili wa Brazil Fernando na Fernandinho kuchezeshwa pamoja kama alivyodokeza Pellegrini.
Pia upo uwezekano mkubwa kwa Kepteni wa City, Vincent Kompany, akacheza Mechi hii baada ya kuwa nje kwa maumivu kwa Mechi kadhaa.
Kutoka huko Madrid, Kocha wa Real, Zinedine Zidane, amebeba Kikosi chake chote kusafiri kwenda Jiji la Manchester akiwemo pia majeruhi Cristiano Ronaldo ambae Jumamosi hakucheza Mechi ya La Liga ambayo Real ilicheza Ugenini na Rayo Vallecano na kutoka nyuma 2-0 na kushinda 3-2.

Kikosini pia yumo Karim Benzema ambae aliumia kwenye Mechi hiyo na Rayo Vallecano na kulazimishwa kubadilishwa katika Kipindi cha Kwanza.