Friday, April 22, 2016

REAL MADRID WAKUBALI KUMKOSA CRISTIANO RONALDO MECHI INAYOFUATA YA RAYO VALLECANO


Cristiano Ronaldo ameumia na ana Maumivu ya Musuli wake wa Mguu umeleta mashaka kwa Staa huyo wa Real Madrid kucheza Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI Uwanjani Etihad Jijini Manchester dhidi ya Manchester City hapo Jumanne.
Tayari Ronaldo, mwenye Miaka 31, amethibitishwa kuikosa Mechi ya Real ya La Liga ya Jumamosi Ugenini na Rayo Vallecano kutokana na maumivu aliyoyapata Jumatano wakati Real inaichapa Villareal 3-0 Uwanjani Santiago Bernabeu.

Kocha wa Real, Zinedine Zidane, amesema hii Leo: “Kesho hatacheza. Tumempima lakini si tatizo kubwa lakini hawezi kucheza. Baada ya hapo tutamtathmini Siku hadi Siku. Tutajua baadae kuhusu Jumanne.”

Msimu huu, Ronaldo, Mchezaji wa zamani wa Manchester United, ameifungia Real Bao 47 katika Mechi 44.