Thursday, April 14, 2016

REFA KEVIN FRIEND MKAZI WA LEICESTER AFUTWA KUICHEZESHA MECHI YA SPURS!

Refa Kevin Friend Ameondolewa kuichezesha Mechi ya Tottenham Hotspur na Stoke Citu itakayochezwa Jumatatu kwa sababu yeye ni Shabiki wa Leicester City inayoongoza Ligi hiyo.
Spurs wako Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 7 nyuma ya Leicester. huku Mechi zikibaki 5 Ligi kumalizika.
The Professional Game Match Officials Ltd, PGMOL, ambao ndio husimamia na kupanga Marefa wa Mechi za Ligi huko England imekuwa haimpi Friend kuchezesha Mechi za Leicester City.
Refa Kevin Friend anaisha huko Leicester na huhudhuria Mechi za Leicester kama mtazamaji kwa utashi wake.
Ikizungumzia kuondolewa kwa Friend kwenye Mechi ya Spurs na Stoke, PGMOL imesema wakati huu si muafaka kwa Refa huyo kusimamia Mechi hiyo.
Taarifa ya PGMOL pia imeeleza pia hawakutaka kuzua mijadala na kukaziwa macho Refa huyo.
Sasa Mechi hiyo ya Jumatatu itasimamiwa na Refa Neil Swarbrick kutoka Preston na Friend amepangiwa kuwa Refa wa Mechi ya Jumanne kati ya Man City na Newcastle.