Monday, April 25, 2016

RIYAD MAHREZ ASHINDA TUZO YA PFA KWA MWAKA 2016.


Riyad Mahrez, Mchezaji kutoka Algeria, amekuwa Mchezaji wa Kwanza kutoka Afrika na Klabu ya Leicester City kutwaa Tuzo ya Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa England, PFA [Professional Footballers' Association].
Mahrez alikabidhiwa Tuzo yake Jana Uiku katika Hoteli ya Grosvenor Jijini London katika Hafla maalum.
Msimu huu, Mahrez amefunga Bao 17 na kutoa msaada wa Bao 11 katika Mechi 34 za Ligi na kuisaidia Leicester City kuongoza Ligi Kuu England wakikaribia kutwaa Ubingwa.

Kwa upande wa Wachezaji Vijana, Dele Alli wa Tottenham, mwenye Miaka 20, ndie amezoa Tuzo ya PFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana.
Nae Winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs, ambae ndie Mchezaji alietwaa Mataji na Tuzo nyingi katika Historia ya Uingereza, Jana alitunukiwa Tuzo ya PFA ya Sifa Maalum.
Mahrez, mwenye Miaka 25, amewabwaga Fowadi wa Tottenham Harry Kane, Kiungo wa Arsenal Mesut Ozil, Kiungo wa West Ham Dimitri Payet na Wachezaji wenzake wa Leicester, Jamie Vardy na N'Golo Kante, na kutwaa Tuzo hii.


-Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa England wa PFA, yaani The Professional Footballers' Association Players' Player of the Year, hutolewa kila Mwaka kwa Mchezaji ambae ndie alikuwa Bora kwa Mwaka mzima huko England.
-Tuzo hii ilianzishwa Msimu wa 1973/74 na Mshindi kwa Kura za Wanachama wa PFA.
PFA TUZO YA SIFA MAALUM - RYAN GIGGS, AIBEBA!
Winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs, ambae ndie Mchezaji alietwaa Mataji na Tuzo nyingi katika Historia ya Uingereza, Jana alitunukiwa Tuzo ya PFA ya Sifa Maalum.
Ryan Giggs, mwenye Miaka 42 na alieichezea Man United Mechi 963, ikiwa ni Rekodi, anafuata nyayo za Malejendari wa Klabu hiyo waliowahi pia kuitwaa Tuzo hii kina Sir Alex Ferguson, Sir Matt Busby na Sir Bobby Charlton.

Hivi sasa Giggs ni Meneja Msaidizi wa Man United na enzi za Uchezaji wake kwenye Klabu hiyo, Giggs alitwaa Ubingwa wa England mara 13, FA CUP mara 4 na UEFA CHAMPIONS LIGI mara 2.
Akipokea Tuzo hiyo, Giggs, ambae alitwaa Tuzo ya PFA ya Mchezaji Bora Mwaka 1992 na 1993, alisema: “Ukitwaa kila Tuzo unatizama hicho Kikombe na kuona Wachezaji waliowahi kukitwaa na unajua hii ni heshima kubwa. Nina bahati kuitwaa na nitafurahia!”