Monday, April 11, 2016

ROMA MKATOLIKI AFUNGA PINGU ZA MAISHA JIJINI TANGA

April 9, 2016 Siku ya jumamosi ni siku ambayo imeingia kwenye historia ya maisha ya Mwanamuziki wa kufokafoka almaarufu HipHop kutoka Nchini Tanzania si mwingine ni Roma Mkatoliki ambae siku hiyo amefunga pingu za maisha na mwandani wake wa siku nyingi ambae walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Ivan.
Pingu za maisha zilifungwa katika Jiji la Mahaba Kule Tanga kunani mara baada ya bibi harusi kuagwa katika jiji la Maraha Na Karaha la Dar Es Salaam february 2016. Pamoja na ndoa hiyo harusi yake ilihudhuliwa na wakali wa bongo fleva wengi tu huku Kala Jeremiah akiwa best man wa Roma Mkatoliki

Kila la Heri Roma Mkatoliki Roma Mkatoliki afunga pingu za maisha Jijini Tanga