Friday, April 1, 2016

SIR ALEX FERGUSON ASEMA VAN GAAL AKIPEWA MUDA ZAIDI NDIPO MAFANIKIO YATAFUATA...SUBIRA YATAKIWA!

BOSI wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amemtetea Meneja wa sasa Louis van Gaal na kusema mafanikio yatarejea Klabuni hapo.
Van Gaal hajatwaa Taji lolote kwa Miaka Miwili ambayo yupo kwenye madaraka lakini nae Ferguson alisubiri Miaka Minne ndipo akatwaa Taji lake la kwanza na kufungua mtiririko wa Makombe kwa kutwaa Vikombe 38 katika Miaka 22 iliyofuatia.
Akiongea na Sky Sports, Ferguson alieleza: “Kwa historia ya Miaka 150, si mbaya kusubiri Miaka kadhaa ya ukame kwani mafanikio yatarejea na yatarudi kwa nguvu tu!”
Aliongeza: “Kama Shabiki wa Manchester United unapaswa uwe na uvumilivu na wameonyesha hilo kwa Miaka mingi tu. Wakati wa Sir Matt Busby, wakati wangu!”
Van Gaal amewahi kutwaa Mataji ya Ubingwa huko Spain, Germany na Netherlands na pia Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Ajax Mwaka 1995.
Lakini tangu Ferguson astaafu Mwaka 2013, Man United walitwaa Ngao ya Jamii tu chini ya David Moyes ambae hakudumu hata Msimu mmoja na kurithiwa na Van Gaal.
Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Timu ya 4 Man City na pia wapo Robo Fainali ya FA CUP ambayo wanapaswa kurudiana na West Ham hapo Aprili 13.

Ferguson amesisitiza ni rahisi kuponda huku akitaja kuwepo kwa majeruhi wengi na pia kuwa na Wachezaji wapya wengi mwanzoni mwa Msimu kuwa ni sababu ambazo ziliwakaba Man United kufanikiwa Msimu huu.Marcus Rashford and Jesse Lingard celebrate victory