Friday, April 1, 2016

SUNDERLAND KUACHANA NA EMMANUEL EBOUE.

Emmanuel EboueKLABU ya Sunderland inajipanga kusitisha mkataba wa beki wao Emmanuel Eboue baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kumfungia mwaka mmoja kutojishughulisha na masuala ya soka. Beki huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye alijiunga na Sunderland Machi 9 mpaka mwishoni mwa msimu huu, alilimwa adhabu hiyo baada ya kushindwa kulipa fedha alizokuwa akidaiwa na wakala wake wa zamani. Sunderland wamesema katika taarifa yao Eboue hakuifahamisha klabu kuhusiana na suala hilo ambalo lilianza toka Julai mwaka 2013. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amepewa wiki mbili kukat rufani kupinga adhabu hiyo.