Thursday, April 21, 2016

TIMU YA MWAKA ENGLAND: 8 WA LEICESTER, SPURS WAITAWALA, WALOBAKI NI 3 WA MAN UNITED, ARSENAL, WEST HAM!

KIKOSI BORA cha Timu ya Mwaka ya England kilichoteuliwa na PFA, Professional Footballers' Association, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa, kimevuja kabla kutangazwa rasmi hapo Jumapili Aprili 24 na kulazimisha PFA kukianika rasmi hii Leo.
Kwenye Kikosi hicho wapo Wachezaji Wanne Wanne wa Timu zinazoongoza Ligi Kuu England, Leicester City na Tottenham Hotspur.
Wachezaji Wanne wa Leicester ni Wes Morgan, N'Golo Kante, Riyad Mahrez na Jamie Vardy na wale wa Spurs ni Toby Alderweireld, Danny Rose, Dele Alli na Harry Kane.

Wachezaji waliobaki ni mmoja moja wa Timu nyingine ambao ni Kipa wa Man United David De Gea, Fulbeki wa Arsenal Hector Bellerin na Mchezaji wa West Ham Dimitri Payet.

Mchezaji wa Arsenal, Mesut Ozil, ambae yuko kwenye Listi ya Wagombea 6 Bora ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA pamoja na Kane, Kante, Mahrez, Payet na Vardy, hayumo kwenye Kikosi hicho.


FAHAMU:
-Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa England wa PFA, yaani The Professional Footballers' Association Players' Player of the Year, hutolewa kila Mwaka kwa Mchezaji ambae ndie alikuwa Bora kwa Mwaka mzima huko England.

-Tuzo hii ilianzishwa Msimu wa 1973/74 na Mshindi kwa Kura za Wanachama wa PFA.

LISTI ZA WAGOMBEA:
-WANAUME:
-Dimitri Payet (West Ham)
-Harry Kane (Tottenham)
-Jamie Vardy (Leicester)
-Mesut Ozil (Arsenal)
-N'Golo Kante (Leicester)
-Riyad Mahrez (Leicester)

-VIJANA:
-Dele Alli (Tottenham)
-Harry Kane (Tottenham)
-Jack Butland (Stoke)
-Philippe Coutinho (Liverpool)
-Romelu Lukaku (Everton)
-Ross Barkley (Everton)

-WANAWAKE:
-Beth Mead (Sunderland)
-Gemma Davison (Chelsea)
-Hedvig Lindahl (Chelsea)
-Izzy Christiansen (Manchester City)
-Ji So-Yun (Chelsea)

-KIJANA KWA WANAWAKE:
-Beth Mead (Sunderland)
-Danielle Carter (Arsenal)
-Hannah Blundell (Chelsea)
-Keira Walsh (Manchester City)
-Nikita Parris (Manchester City)