Tuesday, April 5, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA 2 v 1 ATLETICO MADRID, TORRES NJE KWA KADI NYEKUNDU! SUAREZ AFUNIKA KWA KUIPA BARCA USHINDI!


Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONS LIGI, FC Barcelona wakiwa kwao Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain, walitoka nyuma kwa Bao 1 na kuwafunga wenzao wa Spain Atletico Madrid Bao 2-1 katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Fernando Torres alliipa Bao Atletico Dakika ya 26 lakini akapewa Kadi ya Njano Dakika ya 30 na kuizoa nyingine Dakika ya 37 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Wakicheza dhidi ya Mtu 10 Atletico, Barcelona walisawazisha Dakika ya 63 pale shuti la Neymar kuelekea Golini lilipomaliziwa kibahati na Luis Suarez.
Dakika ya 74 Luis Suarez tena akaona nyavu kwa Kichwa kufuatia Krosi ya Dani Alves na kuwapa Barca ushindi wa 2-1.Kipindi cha pili Barca walisawazishiwa bao na Suarez na kufunga bao tena la pili na kufanya Barca kuwa mbele ya bao 2-1

Fernando Torres of Atletico Madrid is shown a yellow card by referee Felix Brych during the UEFA Champions League quarter final first leg match between FC Barcelona and Club Atletico de Madrid at Camp Nou on April 5, 2016 in Barcelona, Spain.
Torres dakika ya 25 anaipachikia bao la kwanza Atletico Madrid kwa kufanya 1-0 dhidi ya Barca. 
VIKOSI:
Barcelona wanaoanza XI:
Ter Stegen, Alves, Pique, Mascherano, Alba, Busquets, Rakitic, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar
Barca akiba: Bravo, Bartra, Vermaelen, Arda Turan, Rafinha, El Haddadi, Sergi Roberto
Atletico Madrid wanaoanza XI: Oblak, Juanfran, Lucas, Godín, Filipe Luís, Gabi, Saúl, Koke, Carrasco, Griezmann, Torres
Atletico akiba: Moya, Gamez, Kranevitter, Fernandez, Correa, Partey, Vietto 


Barcelona v atletico madrid