Monday, April 4, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA vs ATLETICO MADRID, BAYERN MUNICH v BENFICA

JUMANNE Usiku Mabingwa Watetezi wa UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, FC Barcelona wako kwao Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain kucheza na wenzao wa Spain Atletico Madrid kwenye Mechi ya kwanza ya Robo Fainali
Mechi nyingine ya Robo Fainali Siku hiyo hiyo ni huko Munich, Germany wakati Bayern Munich watacheza na Benfica ya Portugal.
Barcelona wanaingia kwenye Mechi hii na Atletico Madrid wakitoka kwenye kipigo kitakatifu cha Jumamosi Uwanjani kwao Nou Camp mikononi mwa Mahasimu wao wakubwa Real Madrid waliowachapa 2-1 kwenye Mechi ya La Liga.
Kipigo hicho kilukuwa cha kwanza kwa Barca katika Mechi 39 chini ya Kocha Mkuu wao Luis Enrique.
Mbali ya hilo, Barca wanatinga kwenye Robo Fainali hii wakiwania kuwa Timu ya kwanza tangu Miaka ya 1990 kuweza kutetea vyema Taji lao la Ulaya ambalo wao walishindwa kufanya hivyo Mwaka 2010 na 2012.

Lakini Wachambuzi wengi, hasa wa huko Spain, wamekuwa na wasiwasi na Barca kwa sasa baada ya kuonekana wakiwa goigoi walipofungwa Juzi na Real.

BARCELONA v ATLÉTICO MADRID
-Barcelona wameshinda Mechi 6 zilizopita dhidi ya Atletico Madrid lakini katika Mechi yao pekee ya Ulaya, Atletico iliibwaga Barca kwa Jumla ya Bao 2-1 katika Mechi 2 za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI ya Msimu wa 2013/14.
Lakini, Kocha Luis Enrique, mara baada ya kipigo toka kwa Real, amesema: “Tushaisahau Gemu hiyo!”
Ingawa Atletico hawana rekodi nzuri dhidi ya Barca, Timu hiyo ya Jiji la Madrid ni wapinzani wagumu na hasa kwa Mechi za Ulaya na Barca watakumbuka vyema nini walitendewa Msimu wa 2013/14 kwenye UCL.
Kwenye Hatua ya Robo Fainali ya UCL, kama hii, Barca walitoka 1-1 na Atletico Uwanjani Nou Camp na kunyukwa 1-0 huko Vicente Calderon na kutupwa nje ya UEAF CHAMPIONS LIGI.

Hali za Timu
Majeruhi wa Barca ni Mathieu na Adriano na hivyo Luis Enrique ana uwezo wa kushusha Kikosi thabiti.
Kwa upande wa Atletico Madrid, chini ya Kocha Diego Simeone, watafurahia kuwa nae nguzo yao kuu Diego Godin ingawa watamkosa Gimenez ambae pengo lake linaweza kuzibwa na Stefan Savic.
Baada ya Mechi hizi za Jumanne, Jumatano pia zipo Mechi 2 za Robo Fainali za UCL ambapo Paris St-Germain wapo kwao Jijini Paris Nchini France kucheza na Manchester City ya England na nyingine ni huko Germany kati ya Wolfsburg na Real Madrid.
Marudiano ya Robo Fainali hizi ni Aprili 12 na 13.