Wednesday, April 6, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO NI PSG v MANCHESTER CITY


Manchester City vs Paris St-Germain
Hii ni mara ya kwanza kwa Man City kucheza hatua hii ya UCL wakati kwa PSG hii ni mara ya 4 mfululizo kucheza kutua hii.
Timu hizi zimekutana mara 1 tu Ulaya, Desemba 2008, kwenye UEFA CUP Uwanjani Etihad na Mechi kwisha 0-0.
Hii Leo, City wanatarajiwa kuwa nae tena Kipa wao Nambari Wani Joe Hart ambae aliumia Machi 20 walipofungwa na Man United 1-0 kwani sasa yuko fiti.
Akiongea kuhusu Mechi hii, Meneja wa City, Manuel Pellegrini, amesema kila Timu ina nafasi ya kutinga Nusu Fainali na wao hawatacheza Mechi hii ya Ugenini kwa kujihami.
Lakini City itawakosa Yaya Toure na Raheem Sterling ambao ni Majeruhi.
PSG wao wanaweza kumtumia Mchezaji wa zamani wa Man United, Angel Di Maria, ambae alipumzisha Mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Nice ya Ligi 1 waliyoshinda 4-1.

Akizungumzia Mechi hii, Kocha wa PSG, Laurent Blanc, aliewahi pia kuichezea Man United, amsema kila Timu ina nafasi ingawa wao wako juu ya City.
Nguzo kubwa ya PSG ni Mshambuliaji wao kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic ambae amepachika Bao katika Mechi zote 4 zilizopita za UEFA CHAMPIONS LIGI