Wednesday, April 6, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: PSG 2 v 2 MANCHESTER CITY


Paris St-Germain na Manchester City zikitoka Sare huko Mjini Paris, C=VfL Wolfsburg ilifanya maajabu yasiyotarajiwa kwa kuitandika RealMadrid huko Germany katika Mechi za kwanza za Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, kwa Timu hizo.
Hatua hii ilianza Jumanne kwa Mechi 2 na Timu hizi zitarudiana Wiki ijayo ili kupata Timu 4 zitakazotinga Nusu Fainali.
Huko Volkswagen Arena Jijini Wolfsburg Nchini Germany, VfL Wolfsburg, ambayo inasuasua kwenye Bundesliga, iliitandika Real Madrid 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Kwanza.
Bao hizo zilifungwa kwa Penati tata ya Dakika ya 18 iliyotolewa baada yakuamuliwa Casemiro kamchezea faulo Andre Schurrle na Ricardo Rodriguez kufunga huku Bao la Pili kufungwa Dakika ya 25 na Max Arnold.
Timu hizi zitarudiana huko Santiago Bernabeu Wiki ijayo.


Huko Parc des Princes, Jijini Paris Nchini France, PSG walilazimishwa Sare ya 2-2 na Man City matokeoa ambayo yanawapa faida City kwa Bao za Ugenini watakaporudiana huko Etihad Wiki ijayo.
Kwenye Mechi hii, PSG walipata Penati ambayo Zlatan Ibrahimovic alipiga na Kipa Joe Hart kuokoa lakini Ibrahimovic baadae, katika Dakika ya 41 akaipa Timu yake Bao la Kwanza la kusawazisha Bao la kuongoza la City lililofungwa Dakika ya 38 na Kevin de Bruyne. PSG wakapiga Bao la Pili Dakika ya 59 kupitia Rabiot na Fernandinho kuipa Sare Dakika ya 72.

Paris Saint-Germain bao zimefungwa na

Zlatan Ibrahimovic 41
Adrien Rabiot 59'

Manchester City baozimefungwa na

• Kevin De Bruyne 38
• Fernandinho 722-2VIKOSI:
Paris Saint-Germain walioanza XI:
Trapp, Thiago Silva, David Luiz, Aurier, Maxwell, Thiago Motta, Matuidi, Rabiot, Di Maria, Cavani, Ibrahimovic
PSG Akiba: Sirigu, Stambouli, Marquinhos, Lucas, Kurzawa, Van der Wiel, Augustin
Manchester City walioanza XI: Hart, Sagna, Otamendi, Mangala, Clichy, Fernando, Fernandinho, Navas, Silva, De Bruyne, Aguero
Man City Akiba: Caballero, Zabaleta, Demichelis, Kolarov, Delph, Bony, Iheanacho