Friday, April 15, 2016

UEFA EUROPA LIGI-DROO NUSU FAINALI YATOKA: LIVERPOOL vs VILLAREAL

DROO ya Mechi za Nusu Fainali za UEFA EUROPA LIGI imefanyika Leo huko Mjini Basel, Uswisi na Liverpool ya England imepangwa kucheza na Villareal ya Spain.
Liverpool wataanza Ugenini Nyumbani kwa Timu hiyo ambayo iko Nafasi ya 4 kwenye La Liga na ambayo Msimu huu imezichapa Klabu zote za Madrid, Real na Atletico, na pia kutoka Sare na Mabingwa Watetezi FC Barcelona.
Kwenye EUROPA LIGI, Villareal ilizibwaga Napoli, Bayer Leverkusen na Jana kushinda Ugenini walipoitwanga Sparta Prague Bao 4-2 na kuwatupa nje kwa Jumla ya Bao 6-3.
Liverpool wao waliwatoa Vigogo wa England Manchester United na Jana kuibwaga Borussia Dortmund 4-3 na hivyo kusonga kwa Jumla ya Mabao 5-4 kwa Mechi mbili.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Mabingwa Watetezi Sevilla ya Spain na Shaktar Donetsk ya Ukraine.
Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali itachezwa Aprili 28 na ya Pili ni Mei 5.
Fainali ya Mashindano haya ni Mjini Basel, Uswisi hapo Mei 18.