Sunday, April 3, 2016

VPL: LEO YANGA WAPO TAIFA NA KAGERA SUGAR, AZAM WAPO KIRUMBA KUKIPIGA NA TOTO!

LEO Yanga, ambao ni Mabingwa Watetezi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, wanashuka Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Kagera Sugar wakiwania ushindi ili kuikaribia Simba kileleni kwenye Ligi hiyo.
Hadi sasa, Simba bado wanaongoza VPL wakiwa na Pointi 57 kwa Mechi 24 wakifuatiwa na Yanga wenye Pointi 50 kwa Mechi 21 na Azam FC wapo Nafasi ya 3 wakiwa pia na Pointi 50 kwa Mechi 21.
Kagera Sugar wapo Nafasi ya 12 wakiwa na Pointi 25 lakini kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu walichapwa 2-0 na Yanga.
Mechi hii ya Leo ya Yanga pia ni kipimo kizuri kwao kwani Jumamosi ijayo hapo hapo Uwanja wa Taifa watacheza na Al Ahly ya Egypt ikiwa ni Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Pili ya CAF CHAMPIONS LIGI.
Nayo Timu ya 3 ya VPL, Azam FC, ambao wamecheza Mechi 21 na wana Pointi 50 sawa na Yanga, wapo huko CCM Kirumba kucheza na Toto Africans.


Wachezaji wa Kagera Sugar