Sunday, April 24, 2016

WAYNE ROONEY AWATAKA WENZAKE KUWANIA KUBEBA FA CUP!

KEPTENI wa Manchester UnitedWayne Rooney ana hamu kubwa ya kutwaa FA CUP baada ya Jumamosi kuifunga Everton 2-1 Uwanjani Wembley Jijini London na kutinga Fainali ya Kombe hilo ambalo sasa linaitwa EIMRATES FA CUP kwa sababu za kiudhamini.
Jana huko Wembley, Rooney alicheza vizuri kama Kiungo ambapo Bao za Man United zilifungwa na Marouane Fellaini na Anthony Martial na kuwafikisha Fainali yao ya 19 ya FA CUP ambayo ni Rekodi.
Man United wametwaa FA CUP mara 11, wakizidiwa tu na Arsenal waliotwaa mara 12, lakini mara ya mwisho Man United kulitwaa ni 2004.
Kwenye Fainali ya Mwaka huu, ambayo itachezwa Mei 21, Man United watakutana na Mshindi kati ya Crystal Palace na Watford United.
Akiongea, Rooney alisema: “Nimecheza Fainali 2 za FA CUP na zote tulishindwa. Safari hii ni nafasi kubwa kwetu. Itakuwa Fainali ngumu. Lakini Mashabiki watakaokuja Wembley watahitaji mchezo mzuri. Tuna Kikosi mchanganyiko cha Vijana na Wachezaji wapya na tukitwaa Kombe hili utakuwa mwanzo mzuri kwetu!”