Friday, May 20, 2016

AIFF YOUTH CUP: SERENGETI BOYS KUIVAA MALAYSIA JUMAMOSI, KUTINGA FAINALI?

Timu ya Taifa ya Vijana wa Tanzania wa chini ya Miaka 17 Jumamosi huko Tilak Maidan Stadium, Vasco, Goa Nchini India itacheza na Malaysia kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi wakisaka ushindi ili kutinga Fainali ya 2016 AIFF Youth Cup.

Tanzania imeshacheza Mechi 3 na kuifunga India 3-1 na kutoka Sare na USA 1-1 na kisha South Korea 1-1.

Ili kutinga Fainali Serengeti Boys wanapaswa kuifunga Malaysia ambayo imetoka Sare na India na kubondwa na South Korea 3-0.

Ikiwa Serengeti Boys wataifunga Malaysia basi njia yao itakuwa nyeupe ikiwa pia Jumamosi Mechi kati ya USA na South Korea itaisha kwa Timu moja kushinda.

MSIMAMO ULIVYO KWA SASA:

-2016 AIFF Youth Cup ni Mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la India, All India Football Federation (AIFF), mahsusi kuitayarisha Timu yao ya U-17 kwa ajili ya Mashindano ya AFC U-16 na yale ya 2017 FIFA U-17 World Cup.

-Mashindano haya yanachezwa kuanzia Mei 15 hadi Mei 25 huko Tilak Maidan Stadium in Vasco, Goa Nchini India.

-Mashindano haya yana Hatua mbili za Kundi na za Mtoano.

-Timu 4 za juu za Kundi ambalo lina Timu 5 zitasonga kuingia Mtoano ambapo Timu mbili za juu zitacheza Fainali.


AIFF YOUTH CUP

RATIBA/MATOKEO:

15 May 2016
Tanzania 1 vs United States 1
-TANZANIA: Mohamed Abdallah 13', USA: Grant Ogudimu 3'

15 May 2016
India 2 Malaysia 2

17 May 2016
India 1 Tanzania 3

-Komal Thatal, 36' TANZANIA: Maziku Amani Goal 20', Mohammed Sarif Khan 28' (o.g.),

Asad Ali 47'

17 May 2016
Malaysia 0 South Korea 3

19 May 2016
South Korea 2 Tanzania 2

-KOREA: Kim Taehwan 15', Joung Sungjune 58' TANZANIA: Asad Ali Juma 12', Maulid Lembe 87'
 

19 May 2016
United States 4 India 0
21 May 2016
United States v South Korea
21 May 2016
Tanzania v Malaysia
 

23 May 2016
Malaysia v United States
23 May 2016
South Korea v India
Mshindi wa 3
25 May 2016

Mshindi wa 3 wa Kundi v Mshindi wa 4 wa Kundi

FAINALI
25 May 2016

Mshindi wa 1 wa Kundi v Mshindi wa 2 wa Kundi