Tuesday, May 24, 2016

AIFF YOUTH CUP: USA, KOREA FAINALI, SERENGETI BOYS vs MALAYSIA KUSAKA MSHINDI WA 3!

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya Miaka 17, Serengeti Boys, sasa itacheza na Malaysia kwenye Mashindano ya 2016 AIFF Youth Cup yanayochezwa huko Tilak Maidan Stadium in Vasco, Goa Nchini India, kusaka Mshindi wa 3 baada ya Jana USA na South Korea kufanikiwa kutinga Fainali.

Jana USA iliifunga Malaysia 2-1 na South Korea kutoka 0-0 na Wenyeji India na Matokeo hayo yalikamilisha Mechi za Kundi la Timu 5 na kuzipa USA na South Korea Nafasi 2 za juu za Kundi na hivyo kutinga Fainali watakapokutana wenyewe wakati Tanzania sasa imemaliza Nafasi ya 3 na itacheza na Malaysia, iliyomaliza Nafasi ya 4, kugombea Mshindi wa 3.
Juzi Tanzania ilimaliza Mechi za Kundi kwa kutoka Sare 2-2 na Malaysia.
Awali, Serengeti Boys ilitoka Sare 1-1 na USA, kuitandika India 3-1 na kutoka Sare 2-2 na South Korea.
India wametupwa nje baada ya kumaliza mkiani mwa Kundi.

MSIMAMO WA MWISHO WA KUNDI:
-2016 AIFF Youth Cup ni Mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la India, All India Football Federation (AIFF), mahsusi kuitayarisha Timu yao ya U-17 kwa ajili ya Mashindano ya AFC U-16 na yale ya 2017 FIFA U-17 World Cup.
-Mashindano haya yanachezwa kuanzia Mei 15 hadi Mei 25 huko Tilak Maidan Stadium in Vasco, Goa Nchini India.
-Mashindano haya yana Hatua mbili za Kundi na za Mtoano.
-Timu 4 za juu za Kundi ambalo lina Timu 5 zitasonga kuingia Mtoano ambapo Timu mbili za juu zitacheza Fainali.