Friday, May 20, 2016

ARSENE WENGER AINGIA SOKONI YU KARIBU KUMSAINI GRANIT XHAKA KUTUA EMIRATES!

Arsenal wanakaribia kumsaini Kiungo na Kepteni wa Timu ya Germany Borussia Monchengladbach Granit Xhaka.
Tayari Klabu hizo mbili zishafikia maafikiano kuhusu Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Switzerland kwa Dau linaloaminika kuwa ni Pauni Milioni 30.

Xhaka, mwenye Miaka 23, tayari yupo Jijini London kukamilisha makubaliano ya maslahi yake binafsi pamoja na upimwaji afya yake ambao umepangwa kufanyika Wikiendi hii.
Kutua kwa Granit Xhaka kutaimarisha safu ya Kiungo ya Arsenal ambayo sasa itaondokewa na of Mikel Arteta, Tomas Rosicky na, pengine, Mathieu Flamini.

Nyota huyo anakuwa Mchezaji wa kwanza kununuliwa na Arsene Wenger ambae Msimu uliopita alishangaza wengi kwa kutonunua Mchezaji yeyote wa mbele mbali ya Kipa Petr Cech.

Xhaka alitua Borussia Monchengladbach Miaka Minne iliyopita baada ya kung’ara mno akiwa na Klabu ya Nchini kwake FC Basel.