Tuesday, May 24, 2016

CAF CC: DROO YA MAKUNDI YAFANYIKA, YANGA KUNDI A NA TP MAZEMBE!

www.bukobasports.com
DROO ya Mashindano ya Klabu Barani Afrika yale ya CAF CHAMPIONS LIGI na KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF CC, immefanyika Mchana huu huko Cairo, Misri na Wawakilishi wa Tanzania, Mabingwa Yanga, wamepangwa Kundi A la CAF CC.
Yanga, ambayo ndio Timu pekee ya Tanzania kwenye Mashindano ya Kimataifa, ipo Kundi A la pamoja na Mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Congo DR na nyingine ni MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Mechi za Kwanza za Makundi kwa CAF CC zitachezwa kati ya Juni 17 na 19 na za Pili ni kati ya Juni 28 na 29.
Mechi za Makundi zitamalizika Tarehe 23 na 24 Agosti na Washindi Wawili wa kila Kundi kutinga Nusu Fainali.

Ratiba kamili tutaileta baadae.
DROO KAMILI:
CAF Kimbe la Shirikisho:

KUNDI A:

-MO Bejaia (Algeria)
-Young Africans (Tanzania)
-TP Mazembe (DR Congo)
-Medeama (Ghana),

KUNDI B:

-Kawkab (Morocco)
-Etoile du Sahel (Tunisia)
-FUS Rabat, Ahly Tripoli (Libya)
 

Mechi za Kwanza za Makundi kuchezwa  17 na 19 Juni 2016

CAF CHAMPIONS LIGI:
KUNDI A:

-Zesco (Zambia)
-Ahly (Egypt)
-ASEC Mimosas (Ivory Coast)
-Wydad Athletic (Morocco)

KUNDI B:
-Enyimba (Nigeria)
-Zamalek (Egypt)
-ES Setif (Algeria)
-Mamelodi Sundowns (South Africa)