Wednesday, May 18, 2016

CAF CC: YANGA YATINGA HATUA YA MAKUNDI LICHA MBINU CHAFU, KUFUNGWA BAO 1-0, KADI NYEKUNDU, KUPIGWA NA MAWE!

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Leo wametinga Hatua ya Makundi ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho licha ya kufungwa 1-0 na GD Sagrada Esperanca ya Angola huko Dundo, Angola.
Bao la Esperanca hii Leo lilifungwa Dakika ya 25 na Love Kabungula.
Ushindi huu wa Kihistoria wa Mabingwa Yanga umekuwa mtamu mno kwani tangu watue huko Angola wamefanyiwa vitimbwi tele ikiwa pamoja na usafiri wa mashaka kutoka Mji Mkuu Luanda kwenda Dundo umbali wa Kilomita 1,134 (Maili 704), na pia Leo kukutana na Refa ‘mtata’ kutoka Madagascar, Hamada el Moussa Nampiandraza, ambae alitoa Penati mwishoni iliyookolewa na Kipa Deo Munishi ‘Dida’ na pia kumpa Kadi Nyekundu Kepteni Nadir Haroub ‘Cannavaro’ huku Kipa Dida akipigwa Jiwe kwa kuokoa hiyo Penati na kusababisha Mechi kusimama.

TIMU ZILIZOTINGA HATUA YA MAKUNDI:
-Yanga
-TP Mazembe - Congo DR
-MO Bejaia – Algeria
-ES sahel – Tunisia
-Medeama – Ghana


KIKOSI CHA YANGA HII LEO

Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Simon Msuva [Geoffrey Mwashiuya, 90’], Thabani Kamusoko [Deus Kaseke, 69’], Donald Ngoma, Amissi Tambwe [Kevin Yondan, 90’], Haruna Niyonzima

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
Raundi ya Mchujo
Marudiano
Ratiba/Matokeo
(Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2)

Jumanne Mei 17
Stade Gebasien - Tunisia 2 TP Mazembe - Congo Dr (2-2)
ES Tunis - Tunisia 1 MO BAEJAIA - Algeria 1 (1-1)

Jumatano Mei 18
GD Sagrada Esperanca - Angola 1 Yanga – Tanzania (1-2)
CF Mounana - Gabon 1 ES Sahel – Tunisia 0 (1-2)
Medeama - Ghana 2 Mamelodi Sundowns - South Africa 0 (3-3)
Misr Almaqasa - Egypt v Al Ahli - Libya
Marrakech - Morocco v El Merreikh - Sudan
FUS Rabat -Morocco v Stade Malien de Bamako - Mali