Friday, May 13, 2016

CHELSEA YAMPA OFA NYONGEZA KEPTENI TERRY MWAKA 1 BAADA MASHABIKI KUMGUSA!

CHELSEA imetangaza kuwa Kepteni wao John Terry amepewa nyongeza ya Mkataba ya Mwaka nmoja.
Mkataba wa sasa wa Terry, mwenye Miaka 35, unamalizika Juni 30.
Chelsea imesema Nahodha wao huyo na Wakala wake wanatafakari Ofa hiyo ili kumwezesha aendelea kuichezea Timu Msimu mpya ujao chini ya Meneja mpya Antonio Conte.
Mwenyewe Terry Siku zote ameweka wazi nia yake ya kumalizia Soka lake Stamford Bridge ambako alianza kuchezea akiwa Mtoto wa Miaka 14.

Hivi sasa Terry anazo Ofa kadhaa za kwenda kucheza kwenye Supa Ligi ya China ambako kuna mvuto mkubwa wa Fedha na Klabu za huko Shanghai SIPG na Jiangsu Suning zinataka achezee kwao.
Lakini Mashabiki wengi wa Chelsea wameilalamikia Klabu kwa kumtupa Veterani wao Terry ns kudai abakishwe.
Hilo lilidhihirika wazi Juzi Anfield ambako Chelsea ilitoka 2-2 na Liverpool kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo Mashabiki waliinua Mabango kuishinikiza Chelsea imbakishe Kepteni wao.
Akiwa na Chelsea, Terry alieanza kuichezea 1998 ametwaa Ubingwa wa England mara 4, FA CUP 5, UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI, mara moja moja, kwenye Timu ambayo ameichezea zaidi ya Mechi 500.


Hivi sasa Terry yupo Kifungoni Mechi 2 kutokana na Kadi Nyekundu aliyopata walipofungwa 3-2 na Sunderland Wiki iliyopita na kuikosa Mechi na Liverpool na pia hatacheza Mechi ya Jumapili huko Stamford Bridge ambayo ni Mechi ya mwisho ya Msimu dhidi ya Mabingwa wapya Leicester City.
Akimwongelea Terry, Meneja wa muda wa Chelsea Guus Hiddink aneeleza: "Miaka 21 Klabu moja ni kitu kikubwa sana! Ndio maana wanakuwa Malejendari! Kazima uwaenzi Malejendari kwa kizazi kijacho!"