Saturday, May 28, 2016

ENGLAND 2 vs 1 AUSTRALIA: KINDA MARCUS RASHFORD APIGA BAO NA KUWEKA HISTORIA ENGLAND!

Ndani ya Stadium of Light, Uwanja wa Klabu ya Sunderland, Chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford alifunga Bao 1 wakati England inaishinda Australia 2-1 na kuandika Historia ya kuwa Kijana mdogo sana kuifungia Bao England.
Akichezea Kikosi cha Kwanza cha England kwa mara ya kwanza kabisa, Rashford alifunga Bao hilo Dakika ya 3 tu ya Mchezo huku akiwa na Umri wa Miaka 18 na Siku 208 na kuivunja Rekodi ya Tommy Lawton ya Mwaka 1938 alipofunga akiwa Mdogo.
England walifunga Bao lao la Pili kupitia Nahodha wao Wayne Rooney alieingizwa Kipindi cha Pili na kufunga Bao hilo Dakika ya 55.
Bao la Australia lilifungwa Dakika ya 75 kupitia Mchezaji wa England Eric Dier aliejifunga mwenyewe.
Mechi hii ya Kirafiki imetoa mwanya kwa Kocha wa England kupima Wachezaji kabla Jumanne kupunguza Kikosi chake cha Wachezaji 26 kuwa 23 na kuwasilishwa kwa UEFA kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2016 zinazoanza huko France hapo Juni 10.RooneyMile Jadinak