Thursday, May 5, 2016

FARID WA AZAM FC AULA ULAYA

WINGA wa kimataifa wa Tanzania,anayekipiga Azam FC Farid Mussa Malik amefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la pili nchini Hispania maarufu kama Segunda B. Habari hiyo njema kwa soka la Tanzania imeripotiwa na Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo huko Hispania,. Kilichobaki sasa ni vilabu vya CD Tenerife na Azam FC kukaa mezani na kufanya mazungumzo juu ya kuuziana mchezaji huyo anayekipiga pia Taifa Stars.

SASA ni dhahiri kwamba, winga mahiri nchini Farid Mussa Malik anayeichezea Azam FC ya Dar es Salaam, ameingia katika anga za soka la kimataifa.
Hatua hiyo imekuja baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Tanzania kufaulu katika majaribio yake alioyokuwa anafanya katika klabu ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania, Deportivo Tenerife.
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa akisema klabu hiyo sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Azam juu ya kumnunua moja kwa moja mchezaji huyo, badala ya kumtwaa kwa mkopo kama walivyokuwa Wahispania hao.