Tuesday, May 10, 2016

FULL TIME: MBEYA CITY 0 v 2 YANGA

Mabingwa wapya Yanga leo wakiwa huko Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya wameonyesha jinsi gani walivyostahili kuwa Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo kwa kuitwanga Timu ya Nyumbani Mbeya City Bao 2-0 kwenye Mechi pekee ya Ligi hiyo.

Hadi Mapumziko, Yanga, ambao walitwaa Ubingwa wa VPL Msimu huu hapo Juzi huku wakiwa na Mechi 3 mkononi, walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 15 la Vicent Bossou.
Amisi Tambwe aliipa Yanga Bao la Pili Dakika ya 84.
Jumamosi Yanga wanatarajiwa kukabidhiwa Kombe lao la Ubingwa wa VPL ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam watakapocheza Mechi yao ya Ligi na Ndanda FC ambao wamekubali kuuhamishia Mchezo huo wao wa Nyumbani kutoka huko Mtwara na kuchezwa Dar ili kunogesha Sherehe za Ubingwa wa Yanga huku wao wakilipwa gharama zote za Usafiri na pia kunufaika na Geti kubwa la Taifa.