Saturday, May 7, 2016

FULL TIME: NORWICH 0 v 1 MANCHESTER UNITED, MATA AIPA MATUMAINI YA 4 BORA MAN UNITED LEO

Wakicheza huko Carrow Road, Manchester United wameifunga Norwich City Bao 1-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kuleta wasiwasi mkubwa kwa Norwich kushushwa Daraja.
Man United walilazimika kumbadili Anthony Martial kabla hata Mechi haijaanza baada ya Mchezaji huyo kuumia Goti wakati Timu ikipasha moto kabla Mpira haujaanza.
Nafasi ya Martial ilizibwa na Ander Herrera.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.
Katika Dakika ya 71, Pasi ndefu ilimshinda Beki wa Norwich Sebastien Bassong na kumkuta Rooney aliechanja mbuga Golini na kutumia akili kubwa ya kumpa pasi safi Juan Mata aliefunga vizuri.

Ushindu huu umewaongeza matumaini Man United ya kumaliza ndani ya 4 Bora kwani wamejichimbia Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Timu ya 4 Man City ambao Jumapili wanacheza na Arsenal.
Sasa Norwich kubaki Ligi Kuu England ni majaliwa kwani wapo Nafasi ya Pili toka mkiani.