Sunday, May 15, 2016

GONZALO HIGUAIN AWEKA HISTORIA YA MAGOLI SERIE A ITALY, APIGA HAT-TRICK!

GONZALO GERARDO HIGUAIN, Mchezaji wa Argentina aliezaliwa France, ameingia kwenye Vitabu vya Historia huko Italy baada ya Hetriki yake hapo Jana wakati Timu yake Napoli ikiichapa Mtu 10 Frosinone 4-0 na kuiwezesha kutwaa Nafasi ya Pili ya Serie A wakiwa nyuma ya Mabingwa Juventus.
Bao zote 3 za Higuain zilifungwa ndani ya Dakika 19 za Kipindi cha Pili na kumfanya awe Mchezaji wa Kwanza kufikia Bao 36 katika Msimu mmoja wa Serie A na kuivunja Rekodi ya Bao 35 ilyowekwa na Mchezaji wa AC Milan Gunnar Nordahl aliyoiweka Msimu wa 1949/50.
Mbali ya Higuain kuweka Rekodi, Mchezaji mwingine wa Napoli Marek Hamsik alipiga Bao 1 na kufungana na Diego Maradona wote wakiwa na Bao 81 wakiwa Nafasi ya Pili kwa Ufungaji Bao nyingi katika Historia ya Napoli.
Ushindi huu wa Napoli umewapa Nafasi ya Pili kwenye Serie A na kuwanya kuanzia Hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.

Jana Mabingwa Juventus waliitwanga Mtu 10 Sampdoria na baada ya Mechi hiyo yao ya mwisho iliyochezwa Uwanjani kwao Turin walikabidhiwa Kombe lao la Ubingwa walioutwaa mapema Mwezi uliopita.
Bao za Juve zilipachikwa na Paulo Dybala, Bao 2, Patrice Evra, Giorgio Chiellini na Leonardo Bonucci.