Monday, May 30, 2016

HARAMBEE STARS 1 vs 1 TAIFA STARS

Kikosi cha kwanza cha timu ya Soka ya Tanzania -Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Harambee Stars ya Kenya Jumapili.
KWENYE Mechi ya Kitafiki iliyochezwa huko Nairobi Uwanja maarufu wa Moi Kasarni Timu za Taifa za Kenya na Tanzania zilitoka Sare ya Bao 1-1.

Mechi hii ilikuwa ni mahsusi kwa matayarisho ya Mechi zao za Makundi za Kombe la Mataifa ya Afrika AFRICON 2017 za Wikiendi ijayo ambapo Kenya na Tanzania zitakuwa Majumbani kwao kwa Kenya kucheza na Congo na Tanzania kuivaa Egypt.
Kwenye Mechi ya Leo, Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 32v la Elias Maguli na Kenya kusawazisha kwa Penati iliyofungwa na Profeshenali wao anaicheza England Klabu ya Southampton Victor Wanyama.