Saturday, May 28, 2016

HULL CITY 1-0 SHEFFIELD WEDNESDAY, HULL WARUDI LIGI KUU ENGLAND MSIMU 2016/2017, DIAME AFANYA KAZI!

HULL CITY imefanikiwa kurudi tena Ligi Kuu England baada ya Msimu mmoja tu walipoishinda Sheffield Wednseday 1-0 kwenye Fainali ya Mechi za Mchujo ya kusaka Timu ya 3 iliyobakia kupanda Daraja kutoka Championship kwenda Ligi Kuu England. licha ya Jana kufungwa 2-0 na Derby County wakiwa Uwanjani kwao.
Bao la ushindi la Fainali hii iliyochezwa Wembley Jijini London lilifungwa Dakika ya 72 na Mchezaji kutoka Senegal Mohamed Diame kwa Shuti kali la juu kutoka Mita 25.
Ushindi huu na kupanda Daraja kunaihakikishia Hull City mavuno ya Pauni Milioni 175 kwenye Ligi Kuu England Msimu ujao mapato ambayo yameongezeka kwa Timu za Daraja hilo kutokana na Mkataba mpya wa Matangazo ya TV utakaoanza Msimu ujao unaoanza Agosti 15.
Hull City, chini ya Meneja Steve Bruce Mchezaji wa zamani wa Man United, sasa wanaungana na Mabingwa wa Championship Burnley na Timu ya Pili Middlesbrough kupandishwa Daraja toka Championship kwenda BPL, Ligi Kuu England Msimu ujao unaoanza Agosti.Mohamed Diame dakika ya (72') aliipatia bao la ushindi Timu yake ya Hull na kuirudisha Ligi kuu kwa kuichapa timu pinzani ya Sheffield Wednesday. Bao hilo lilidumu dakika 90 na hivyo kuipandisha Timu ya Hull City English Premier League tena kutoka Championship kwenye Uwanja wa Wembley.Shangweee!