Saturday, May 14, 2016

HULL CITY YAICHAPA 2-0 DERBY COUNT NA KUJIWEKA SAFI KUPANDA LIGI KUU ENGLAND MSIMU UJAO!

DERBY COUNTY wakiwa Uwanjani kwao Uwanjani kwao Ipro Stadium wamejiweka pabaya kutinga Fainali ya Mechi za Mchujo kusaka Timu ya 3 iliyobakia kupanda Daraja kutoka Championship kwenda BPL, Ligi Kuu England baada ya kufungwa na Hull City Bao 3-0.
Hadi Mapumziko Hull City walikuwa mbele 2-0 kwa Bao za Dakika za 30 na 40 za Abel Hernandez na Jason Shackell, Bao la kujifunga mwenyewe.
Dakika ya 98 Hull City walipiga Bao la 3 kupitia Andy Robertson.

Wiki iliyopita, Middlesbrough iliungana na Burnley kupandishwa Daraja toka Championship kwend BPL, Ligi Kuu England na Nafasi ya 3 na ya mwisho kwa Timu kupanda BPL inapatikana baada ya Mechi za Mchujo zinazohusisha Timu zilizomaliza Nafasi za 3 hadi za 6 ambazo ni Sheffield Wednesday, Brighton, Derby County na Hull City.
Jana Usiku Sheffield Wednesday waliichapa Brighton 2-0 katika Mechi nyingine ya Mchujo.
Marudiano ya Mechi hizi ni Jumatatu na Jumanne ijayo. 

 CHAMPIONSHIP
Mechi za Mchujo
Ratiba/Matokeo:
Ijumaa Mei 13

Sheffield Wednesday 2 Brighton 0
Jumamosi Mei 14
Derby Count 0 vs Hull City 2
Marudiano
Jumatatu Mei 16

2145 Brighton vs Sheffield Wednesday [0-2]
Jumanne Mei 17
21:45 Hull City vs Derby County

Fainali
Wembley Stadium, London
Jumamosi Mei 28 Saa 19:00