Friday, May 13, 2016

JAMIE VARDY MCHEZAJI BORA WA MSIMU LIGI KUU ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa Leicester City, Jamie Vardy ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu baada ya kuiongoza vyema klabu hiyo mpaka kutwaa taji la Ligi Kuu. Klabu hiyo inayotoka East Midlands ambayo ilitangaza tuzo hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter leo, walitwaa taji hilo katika hali ya kushangaza kutokana na kutopewa nafasi kabisa mwanzoni mwa msimu. Vardy pia anafukuzia tuzo ya kiatu cha dhahabu inayotolewa kwa mfungaji bora wa ligi, akiwa amefunga mabao 24 mpaka sasa bao moja nyuma ya Harry Kane wa Tottenham Hotspurs huku kukiwa kumebaki mechi moja kabla msimu kumalizika.Leicester wanatarajia kuwafuata mabingwa wa msimu uliopita Chelsea wakati Spurs wao watakwenda kwa Newcastle United ambao tayari wameshashuka daraja.